HabariMilele FmSwahili

Mtu mmoja afariki katika ajali ya barabarani eneo la Mukaa kaunti ya Makueni

Mtu mmoja amefariki papo hapo huku wanafunzi kadhaa wa shule ya msingi ya Light Academy eneo la Sultan Hamud, wakinusurika baada ya basi lao kuhusiaka katika ajali ya barabarani huko , Mukaa kaunti ya Makueni. Akithibitisha ajali hii, OCPD wa Mukaa Charles Muthui amesema dereva wa basi hilo alifariki baada ya kupoteza mwelekeo na kugonga lori, kabla ya kuanguka na kubungirika mara kadhaa. Wanafunzi wote waliopata majeraha madogo madogo wamekimbizwa katika hospitali moja Sultan Hamud kupokea matibabu.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.