HabariPilipili FmPilipili FM News

Polisi Wawili Wahofiwa Kuuawa Na Wahuni Mombasa.

Maafisa wawili wa polisi wanahofiwa kuuawa baada ya kudungwa kisu na wahalifu katika eneo bunge la Kisauni jana usiku.

Inaarifiwa kuwa polisi hao walitolewa katika kitengo maalum na kupelekwa eneo la Dog section Kisauni.

Baadhi ya taarifa tulizopokea ni kwamba maafisa hao wawili walikwenda eneo hilo kushika doria wakiwa peke yao kabla ya kukumbana na mauti yao.

Wakuu wa polisi wanatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na kisa hicho.

Show More

Related Articles