HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuamua kuhusu ukaguzi wa wahasibu na maafisa wa ununuzi wa idara za serikali

Mahakama ya Nairobi inatarajiwa kutoa uamuzi leo kuhusu hatima ya maafisa wa ununuzi na wahasibu wa idara za serikali walioagizwa kujiondoa afisini ili kukaguliwa upya katika vita dhidi ya ufisadi. Wiki iliyopita mahakama ya leba ilisitisha ukaguzi huo kufuatia kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtata akidai serikali inawalenga maafisa wasiokuwa na hatia. Kauli hii hata hivyo imepingwa na mwanasheria mkuu wa serikali Ken Ogeto. Jaji Onesmus makao atatoa uamuzi baada ya serikali kufeli kupama mwafaka na Okiya nje ya mahakama.

Show More

Related Articles