People Daily

Tahadhari Ya Mikurupuko Ya Maradhi Manne hapa Nchini Yatolewa.

Wizara ya afya imetoa tahadhari ya mikurupuko ya maradhi katika kaunti mbali mbali nchini.

Mkurugenzi wa huduma za matibabu Jackson Kioko amesema mikurupuko ya  maradhi manne yameripotiwa humu nchini tangu mwezi January mwaka huu.

Maradhi hayo ni kama vile Kipindipindu, Ukambi, Chikungunya na homa ya Rift Valley.

Amesema serikali inajitahidi kukabiliana na mikurupuko hiyo katika kaunti zilizoathirika ambapo takriban visa 4,954 za kipindupindu zimeripotiwa tangu januari huku vifo 75 vikiripotiwa.

Kunti hizo ni Mombasa, Garissa, Siaya, Tanariver, Kilifi, Niarobi, Meru, busia, Kirinyaga miongoni mwa nyingine.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.