HabariMilele FmSwahili

Watu 75 wafariki mwaka huu kutokana na kipindupindu

Watu 75 wamefariki maeneo kadhaa nchini tangu mwanzoni mwa mwaka huu baada yao kuugua kipindupindu. Wizara ya afya inasema imenakili zaidi ya visa elfu 4,954 kipindi hicho. Kaunti 19 zimerekodi kuwepo ugonjwa huo 10 miongoni mwa kaunti hizo zikionyesha kushindwa kuudhibiti. Kuhusu homa ya RityValley iliyozuka kaunti ya wajir, wizara hiyo inasema tangu mkurupuko huo juni 7, ni watu 5 wamefariki huku visa 15 vikiripotiwa. Maambukizi mengine wizara hiyo inasema inashughulikia ni maambukizi ya ukambi na chikungunya. Wizara hiyo kadhalika inasema mikakati imewekwa kuzuia maafa zaidi sawa na kuzuia maambukizi zaiadi nchini. Umma pia umetahadharishwa kuwa makini na kuzuru hospitali wanaposhuku wanaugua magonjwa hao.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.