HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 33 wasakata ya NYS kuendelea kuzuiliwa

Washukiwa 33 wa sakata ya kupotea shilingi bilioni 9 za shirika la NYS wataendelea kuziliwa. Ni baada ya hakimu wa mahakama ya ufisadi Douglas Ogot kuagiza kesi hiyo kuanza kusikizwa rasmi tarehe 20 mwezi huu. Aamedinda kukubali ombi la kuwaachilia washukiwa kwa dhamana walivyotaka,akielezwa kuwa tayari mahakama kuu imesema itatoa uamzi wake tarehe 19 mwezi huu.

Hata hivyo Ogot ameridhia ombi la wakili wa mshukiwa Lucy Ngirita pamoja na washukiwa wengine ambao afya zao zimedorora kupata matibabu ya dharura.

Aidha,mawakili wa washukiwa wakiongozwa na Clicff Ombeta wametaka kiongozi mkuu wa uchunguzi katika kesi hiyo Julius Muia kushtakiwa baada ya mshukiwa Jeremiah Ngirita kudai wamekua wakishirikiana kusambaza bidhaa tofauti kwa NYS. Inadaiwa tayari Muia amepewa uhamisho huku naibu wake akiagizwa kuongoza uchunguzi huo.

Show More

Related Articles