HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuamua kuhusu ombi la washukiwa 46 wa NYS kuachiliwa kwa dhamana

Mahakama ya Milimani wakati huu inaandaa vikao vya kusikiliza ombi la washukiwa 46 wa sakata ya NYS wanaotaka kuachiliwa kwa dhamana. Washukiwa hao wamekuwa rumande tokea wiki iliyopita baada ya hakimu Douglas Ogoti kutupilia mbali ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana kutokana na uzito wa tuhuma zinazowakabili. Upande wa mashitaka umekatalia mbali ombi lao ukidai kuwa baadhi ya washukiwa huenda wakashawishiwa na wakubwa wao kuhusiana na mwelekeo wa kesi hiyo.

Show More

Related Articles