People Daily

Matatu 15 Zatolewa Kubeba Waislamu Siku Ya Eid.

Kwa mwaka wa tatu sasa, chama cha wenye matatu pwani kitatoa matatu 15 za kuwabeba waumini wa dini ya kiislamu kuenda kuswali swala ya eid katika uwanja wa Ronald Ngala.

Akiongea na wanahabari, mshirikishi wa chama hicho Salim Mbarak amesema matatu hizo zitapelekwa katika vituo vitano kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi kabla ya swala ya eid kuanza.

Wakati huo huo amesema matatu zitahudumu hadi mwendo wa saa saba usiku wakati wa shamrashamra za sikukuu ya Eid.

Sikuu kuu ya eid ulfitr inatarajiwa kuwa ijumaa ua jumamosi wiki hii ikitegemea kuandamana kwa mwezi.

Show More

Related Articles