HabariMilele FmSwahili

Mawaziri Margret Kobia na Sicily Kariuk kuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu sakata ya NYS

Waziri wa jinsia na masuala ya vijana Prof Margret Kobia na waziri wa afya Sicily Kariuki sasa wamehitajika kufika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu uhasibu kutoa mwangaza zaidi kuhusiana na ukaguzi wa hesabu za serikali katika shirika la huduma kwa vijana NYS. Kariuki ambaye alikuwa akishikilia wizara hiyo kipindi ambacho fedha zinadaiwa kupotea ameagizwa kufika mbele ya kamait hiyo ili kuelezea anachofahamu kuhusiana na sakata hiyo ya shilingi bilioni 9. Kumekuwa na shinikizo za kumtaka waziri Kariuki kuwajibikia sakata hiyo hasa kutoka kwa wabunge wanaodai huenda anaufahamu kuhusu kilichojiri katika asasi hiyo.

Show More

Related Articles