HabariSwahili

Mkurugenzi wa shule Kitengela akamatwa kwa kumshambulia mzazi

Naibu mkurugenzi wa shule ya upili ya Kitengela John Kahora anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kitengela kaunti ya Kajiado, baada ya kudaiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya mama mzazi Jumamosi iliyopita.
Mzazi huyo alikuwa amepokea simu kutoka kwa usimamizi wa shule hiyo waliomtaka ajiwasilishe shuleni upesi kwani mwanawe wa kike alidaiwa kukusudia kujitoa uhai.

Mkurugenzi huyo amekanusha kumpiga mzazi huyo na kudai kuwa mwanamke huyo aliumizwa na lango kuu la shule hiyo.

Show More

Related Articles