HabariMilele FmSwahili

Rais kurejea nchini baada ya kumaliza ziara rasmi nchini Canada

Rais Uhuru Kenyatta ataondoka jijini Quebec nchini Canada leo kurejea nchini baada ya kukamilisha ziara rasmi nchini humo jana. Rais aliyekuwa nchini Canada kuhudhuria kongamano la nchi saba zilizostawi kiuchumi za G7 alikamilisha ziara yake kwa kufanya mashauriano na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau. Viongozi hao wawili waliafikiana kuimarisha uhusiano wa Kenya na Canada katika sekta za biashara na uchumi. Rais Kenyatta kadhaliika amepongeza tangazo la Trudeau kuwa Canada kwa ushirikiano na mataifa ya G7 itatoa dola bilioni 2.9 kufadhili elimu ya wasichana katika mataifa maskini ulimwenguni.

Show More

Related Articles