HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Rais Kenyatta Akutana Na Viongozi Wa Africa Kwenye Mkutano Wa G7.

Rais Uhuru Kenyatta ameungana na viongozi wa nchi za afrika katika kongamano la mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani ya G7, ambapo wamezungumzia jinsi ya kulinda bahari,kukuza   biashara na kuimarisha utulivu wa kikanda.

Katika mazungumzo na Rais Macky Sall wa Senegal, rais Kenyatta amemwomba rais huyo wa Senegal  ruhusa ya kufungua ubalozi mpya jijini Dakar ndani ya miezi 4, ili kuimarisha biashara na mahusiano baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili.

Rais Kenyatta  na  rais wa Rwanda Paul Kagame kwa upande mwingine wameegemea pakubwa mazungumzo ya usalama wa kikanda,biashara,mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na kuunganisha   afrika mbele ya kongamano hilo.

 

Show More

Related Articles