HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wachunguzi wana kibarua kigumu kutanzua ajali hiyo ya ndege

Huku maswali mengi yakijitokeza kuhusiana na ni nini haswa kilisababisha ajali ya ndege iliyoua abiria wanane na marubani wawili mamlaka ya safari za ndege nchini sasa imeonya dhidi ya kueneza fununu kuhusu ajali hiyo na badala yake kukipa nafasi kikosi cha uchunguzi kufanya kazi yake.
Tayari wapekuzi wa ajali za ndege wameanza uchunguzi katika eneo ilimotokea ajali hiyo na wanatarajiwa kuchukua vipande vya mabaki ya ndege hiyo ili kufanya uchunguzi wa kina lakini kibarua kinatarajiwa kuwa kigumu.

Show More

Related Articles