HabariMilele FmSwahili

Watu wote 10 waliokuwa katika ndege ya Fly Sax wafariki

Abiria wote 8 na marubani 2 wa ndege iliyoanguka mlima Abadares kule Kinangop wamepatika wamefariki. Katibu katika wizara ya uchukuzi Paul Maringa anasema amepokea tarifa hiyo kutoka kwa makundi yaliyotambua mabaki ya ndege hiyo ambao wamewapata watu wote 10 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki.
Shughuli ya kuondoa miili hiyo imeanza, kikosi kinachongoza shughuli hiyo kikisema shughuli hiyo huenda ikachungua muda kutokana na ukungu katika mlima ilipo miili ya 10 hao

Show More

Related Articles