HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanafunzi Ambao Wanajihusisha Na Uharibifu Wa Mali Ya Shule Waonywa.

Kamishna wa Kaunti ya Kilifi Magu Mtindika ametoa onyo kali kwa wanafunzi wanaojihusisha na uharibifu wa mali za shule  kwamba hatua kali za kisheria zitawakabidhi dhidi yao.

Hatua hii inajiri baada ya  visa vya uchomaji na uharibifu wa mali za shule kuripotiwa katika shule ya upili ya Chumani na ile ya Galana kwenye Kaunti hiyo.

Mtindika pia amewataka wazazi kufuatilia kwa makini mwenendo ya watoto wao wakiwa nyumbani na kutosita kuarifu vyombo vya usalama kuhusiana na  watoto wanaowashuku.

Show More

Related Articles