HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Matatu Ambazo Zimeinuka Nyuma Kuchukuliwa hatua.

Huenda madereva ambao wameweka spring matatu zao za abiria hapa mjini Mombasa wakajipata pabaya hivi karibuni.

Hii ni baada ya idara ya trafiki kutangaza kuanzisha msako wa matatu hizo ambazo zimeinuka kwa nyuma.

Akizungumza katika mkutano uliowaleta pamoja wadau katika sekta ya usafiri, kamanda wa trafiki nchini Samuel Kimaru amesema magari hayo yako katika hatari kubwa ya kufanya ajali.

Kimaru amewaonya pia madereva ambao hawana vibali kamili akisema watakaopatikana watakamatwa

Show More

Related Articles