HabariPilipili FmPilipili FM News

Ndege Moja Aina Ya FLYSAX Yapotelea Hewani.

Ndege hiyo ya Cesna C208 yenye nambari ya usajili 5y-CAC kutoka Kitale ilipoteza mawasiliano na chumba cha mawasiliano mwendo wa saa kumi na moja jana jionikatika eneo la  Aberdares kilomita 60 kutoka uwanja wa ndege wa jomo Kenyatta.

Ndege hiyo iliondoka kitale kuelekea Nairobi muda mfupi baada ya saa kumi alasiri na ilikuwa na abiria 8 na wahudumu wawili.

Shughuli za kuitafuta zinatarajiwa kuendelea tena asubuhi hii baada ya kutatizwa na mawingu jana jioni.

 

Show More

Related Articles