HabariMilele FmSwahili

Kundi la kwanza la madaktari kutoka Cuba wawasili nchini

Kundi la kwanaza la madaktari 50 kutoka nchini Cuba wamewasili nchini. Naibu mwenyekiti wa kamati ya afya ya baraza la magavana gavana wa Kisumu Anyang Nyongo pamoja na katibu wa usimmaizi katika wizara ya afya Rashid Aman waliwapokea madaktari hao katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Madaktari hao wanatarajiwa kupokea mafunzo katika chuo cha mafunzo ya serikali kabla ya kutumwa katika kaunti mbali mbali. Kundi la pili la madaktari 50 linatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi
Kulingana na Aman aidha madaktari 50 kutoka humu nchini watatumwa Cuba kwa mafunzo maalum ya miaka miwili.

Show More

Related Articles