HabariPilipili FmPilipili FM News

Ishara Za Mawasiliao Za Ndege Fly540 Zaonyesha Iko Sehemu ya Aberdares

Ishara za simu kutoka kwa ndege ya Fly540 iliyopotea Jumanne jioni zimebainisha kuwa ndege hiyo  iko katika  eneo la Aberdares kauti ya Nyandarua.

Mkurugenzi msaidizi wa huduma za wanyamapori anayeongoza kwenye maeneo yenye Milima Simon Gitau ametoa tarifa kwa  Taifa kuwa wanazingatia utafutaji katika eneo la Kinangop, ambapo ishara zilipatikana.

Gitau amesema wameanza tena shughuli ya kuitafuta ndege hiyo saa 10 asubuhi, baada ya kusimamishwa hiyo jana usiku, lakini utafutaji huo unakumbwa na changamoto kutokana na hali mbaya ya anga.

Ndege ya hiyo ya Cesna C208, yenye nambari ya usajili 5Y-CAC, ilikuwa ikitoka  Kitale kaunti ys Trans-Nzoia wakati ilipoteza mawasiliano na mnara wa mkuu wa kudhibiti mawasiliano saa 5:00 jioni eneo la Aberdares.

 

Show More

Related Articles