HabariMilele FmSwahili

KENPHIA : Maambukizi ya virusi vya HIV nchini yangali juu

Kenya bado haijapiga hatua za kuvutia katika vita dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya HIV. Shirika la KENPHIA linaloshughulia utafiti wa virusi hivyo nchini linasema mwaka 2016, asilimia 71 ya watu waliopatikana na virusi hivyo ni kutokana na maambukizi mapya. Ni takwimu mkurugenzi wa maswala ya kiufundi katika shirika hilo Jesica Justman anasema inatia hofu. Anasema uchunguzi huu utakoanza juma lijalo, unawalenga wakenya elfu 45 katika kaunti zote 47 kwa muda wa miezi 6 ijayo.

Justman anasema matokeo ya uchunguzi huo yatasaidia serikali kutafuta njia mpya za kukabili na uhamasisha wakenya dhidi ya kujikinga na maambukizi hayo

Show More

Related Articles