HabariMilele FmSwahili

Usimamizi wa Kenya Pipeline wapuuza madai kuhusu sakata ya bilioni 95

Usimamizi wa kampuni ya Kenya Pipeline umepuuza madai kuhusu sakata ya shilingi bilioni 95 katika kampuni hiyo. Maneja mkurugenzi wa KPC Joe Sang amesema madai hayo hayana msingi ikizingatiwa kuwa mapato ya kampuni hayo kwa mwaka ni takribani shilingi bilioni 28. Kadhalika Sang ametaja madai hayo kuwa yanayonuia kuhujumu utendakazi wa wakuu wa shirika hilo.

Sang pia amepinga madai kuwa baadhi ya kandarasi za kampuni hizo zilitolwewa kinyume na sheria kati ya Agosti mwaka 2016 na Machi 2017. Duru zinasema baadhi ya kandarasi hizo ni ile ya shilingi bilioni ya kiwanda cha kampuni hiyo mjini Mombasa.

Hata hivyo amedhibitisha kuwa baadhi ya maafisa katika kampuni hiyo wanachunguzwa kuhusiana na madai hayo na kuwa kampuni hiyo iko inaunga mkono uchunguzi huo.

Show More

Related Articles