HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kuelekea nchini Canada kuhudhuria kongamano la G7 leo

Rais Uhuru Kenyatta anaondoka nchini leo kuelekea nchini Canada. Rais Kenyatta ni miongoni mwa wakuu wa mataifa na serikali waliopokea mwaliko wa waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau kuhudhuria kongamano la nchi zilizostawi kiuchumi wa G7. Mkutano huo utakaoandaliwa Alhamisi na Ijumaa wiki hii utaangazia maswala ya mabadiliko ya tabianhi, usalama na biashara. Viongozi wa Ufaransa, Marekani, China, Japan, Ujerumani, Uingereza na Italia watahudhuria mkutano huo.

Show More

Related Articles