HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wakuu wa uagizaji bidhaa serikalini na wahasibu waagizwa wajiondoe

Mamia ya wakuu wa idara za ununuzi na uhasibu katika wizara na mashirika ya kitaifa sasa wameamrishwa kuondoka ofisini kwa muda kuruhusu uchunguzi kufanywa dhidi yao kutokana na agizo la rais la kupambana na ufisadi.

Serikali aidha inawataka maafisa hao kuwasilisha tawasifu zao kwa afisi ya mkuu wa utumishi wa umma kufikia ijumaa wiki hii.

Haya yanajiri wakati ufichuzi katika shirika la usambazaji mafuta la Kenya Pipeline umeashiria kwamba baadhi ya maafisa wakuu wa shirika hilo walifuja mabilioni ya pesa kupitia wizi wa mafuta pamoja na zabuni zinazotiliwa shaka.

Show More

Related Articles