HabariPilipili FmPilipili FM News

Omba Omba Wa Ondolewa Katikati Mwa Mji Wa Mombasa.

Takriban omba omba 11 wameondolewa katikati mwa mji wa Mombasa katika msako ulioanzishwa na serikali ya kaunti ya Mombasa wa kuwaondoa barabarani.

Akiongea na wanahabari, mkurugenzi wa kitengo cha Inspektorate Mohammed amir amesema msako huo umeanzishwa ili kuwahakikisha ombaomba hao usalama wao na hata usalama wa wananchi akisema watatafutiwa sehemu mbadala.

Amesema wanashirikiana na idara ya vijana na jinsia pamoja na mashirika mengine kuhakikisha kuwa ombaomba ambao ni watoto wanapelekwa shuleni badala ya kuwa barabarani.

Show More

Related Articles