HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanafunzi Abakwa Shuleni, Kaunti Ya Nairobi.

Wakuu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, kaunti ya Nairobi wanatarajiwa kuendelea kuhojiwa na maafisa wa upelelezi baadae leo, kufuatia kisa cha kubakwa kwa mmoja wa wanafunzi shuleni humo.

Tayari shule hiyo imefungwa kwa kipindi cha wiki moja huku Waziri wa Elimu Amina Mohammed akisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa fursa kwa wizara yake kwa ushirikiano na maafisa wa usalama kuendesha uchunguzi wao kuhusu kisa hicho.

Aidha, Amina ameahidi kuhakikisha shule zote za kutwa zina ulinzi wa kutosha huku akiwahakikishia wazazi kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa masomo yanaendelea jinsi ilivyoratibiwa.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mwanafunzi huyo wa kidato cha pili alivamiwa na mtu ambaye wanafunzi hao wanadai kumjua, alipokuwa akielekea msalani nje ya bweni lao.

Show More

Related Articles