HabariSwahili

Githeri Man amejiwasilisha katika kituo cha kurekebisha tabia ili asaidike

Huku wakenya wakisherehekea siku hii ya Madaraka kote nchini ,
Martin Kamotho, ama kwa jina la utani, ‘Githeri Man’ , mwanamume aliyesifika wakati wa kupiga kura akiwa amebeba lishe la Githeri kwenye foleni ya kupiga kura vilevile amesherehekea siku hii kivyake huku akianza safari mpya katika maisha yake.
Haya yanajiri baada ya Githeri Man kujitosa kwa hulka za unywaji pombe jambo ambalo limeathiri maisha yake sana.
Kwa sasa atakua kwenye  kituo cha kurekebishia tabia cha Mama Care katika kaunti ya Kiambu.Mwanahabari Kimani Githuku alijiunga naye na kutuandalia taarifa hii.

Show More

Related Articles