HabariPilipili FmPilipili FM News

Mchele Ulioharibika Wanaswa Katiaka Eneo La Shimanzi, Mombasa

Takribani magunia 1,110 ya Michele yamenaswa na polisi katika maghala ya shimanzi baada ya kuripotiwa kupakiwa tena na kupelekwa sokoni licha ya kuwa mchele huo ulikuwa uharibike tangu mwezi wa tisa mwaka jana kwa mjibu wa tarehe iliyokuwa kwenye magunia hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi  wa uzani na upimaji wa bidhaa nchini  Micheal Onyancha  amesema washukiwa walikamatwa wakiwa wanabadilisha tarehe ya siku ya kuharibika.

Aidha amewaomba wananchi wanunue bidhaa zilizo na nembo za tarehe ya kutengenezwa na tarehe ya kuharibika ili kujiepusha na maradhi kama vile saratani zinazosababishwa na bidhaa zilizoharibika.

Haya yanajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kuamrisha bidhaa kama hizo kuharibiwa

Show More

Related Articles