HabariPilipili FmPilipili FM News

Madereva Wa Matrela Wajiburudisha Na Watoto Wa Shule Kaunti Ya Kilifi.

Viongozi wa usalama wametakiwa kuingilia kati na kukomesha biashara ya bodaboda kwa watoto wa shule na madereva wa matrela mabao wanawatatiza watoto wa kike.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Mwereni huko Mariakana kaunti ya Kilifi Florence Kirengo,madereva wa malori wamekuwa wakijihusisha na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike na kuwatatiza kimasomo huku wanafunzi wa kivulana wakishiriki biashara ya bodaboda punde tu wanapoenda kwa likizo.

Aidha amesema juhudi zao za kukomesha biashara hiyo bado zinakumbwa na changamoto kwa kuwa shule hiyo iko mjini.

Mbali na hayo mwalimu huyo pia ameitaja miundo misingi duni kama changamoto mojawapo na akaitaka serikali ya kitaifa kuchukua hatua ya haraka ili kutatua shida hiyo.

Show More

Related Articles