HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Joho Amualika Rais Kenyatta Mombasa Kuhubiri Amani.

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amemuomba rais Uhuru Kenyatta kutembelea kaunti ya Mombasa ili kuendeleza harakati za kuhubiri amani na utangamano miongoni mwa wananchi.

Akiongea wakati alipotembelewa na seneta wa kaunti ya Baringo Gedion Moi, gavana Joho amesistiza ipo haja ya viongozi wote Kenya nzima kuendeleza kuwaleta wakenya pamoja.

Kwa upande wake seneta Gedion Moi amedokeza kuwa yuko tayari kutembea na Joho kuhubiri amani kote nchini.

 

Show More

Related Articles