HabariMilele FmSwahili

Wanaharakati waandamana jijini Nairobi kulalamikia kukithiri kwa visa vya ufisadi nchini

Wanaharakati wa mashirika ya kijamii watashiriki maandamano hapa jijini wakilenga kutuma ujumbe wa wananchi kwa serikali kuhusiana na kukithiri visa vya ufisadi. Ni maandamano ambayo yataanzia eneo la Freedom Corner na kuelekea barabara kadhaa za jiji waandalizi wakisema wanalenga kuonyesha gadhabu zao kutokana na ufisadi ambao umepelekea kuporwa raslimali za umma. Maandamano haya yamechochewa na visa vya hivi unde vya kupotea mabilioni ya pesa katika shirika la huduma kwa vijana NYS, ununuzi wa mahindi kwa bodi ya nafaka na mazao NCPB pamoja na sakata zingine.

Show More

Related Articles