HabariMilele FmSwahili

Maafisa wa bodi ya NCPB kuhojiwa na kamati ya kilimo kuhusu sakata ya mahindi leo

Maafisa wa bodi ya nafaka na mazao NCPB watafika mbele ya kamati ya kilimo leo kuhojiwa kuhusiana na sakata ya mahindi katika bodi hiyo. Kamati hiyo inayoongozwa na Adan Ali, inatarajiwa kupata ufafanuzi zaidi kuhusu kwanini baadhi ya wakulima walilipwa mapema ilhali kuna wengine ambao walichelewa kuliipwa baada ya kupeleka mahindi yao kwenye bodi hiyo. Mkao huu unakujia siku moja baad aya waziri wa kilimo Mwangi Kiunuri kufika mbele ya kamati hiyo na kufichua majina mengine 63 ya madalali ambao wanakisiwa kujipatia mamilioni ya fedha katika sakata ya ununuzi wa mahindi.

Show More

Related Articles