HabariMilele FmSwahili

Kaunti ya Makueni yatenga milioni 311 kukarabati barabara zilizoharibiwa na mafuriko

Serikali ya kaunti ya Makueni imetenga shilingi milioni 311, kutengeneza barabara 60 za kaunti zilizo haribiwa na mvua ya masika iliyopita. Serikali hii imeteuwa barabara 2 kati ka kila wadi kaunti ya Makueni ikiwa na wadi 30 pale ambapo zinajumuisha barabara 60 zote zitakazokatwa wakati huu. Akizungumza wakati wa kuanzisha zoezi hili katika wadi ya Kiima Kiu Kalanzoni gavana amewaimiza wale watapewa kandarasi hii wahakikishe wamefanya kazi pamoja na kamati zilizoteuliwa kusimamia shughuli hiyo.

Show More

Related Articles