HabariMilele FmSwahili

Rais na Naibu wake kuongoza hafla ya maombi ya kitaifa jijini Nairobi

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto leo wataliongoza taifa katika hafla ya 16 ya maombi ya kitaifa inayoandaliwa hapa jijini Nairobi. Wabunge na maseneta magavana, viongozi wa kidini watajumuika na wajumbe kutoka matiafa ya Afrika mashariki Uingereza na Marekani katika hafla hii. Kauli mbiu ya mwaka huu inaambatana na juhudi za kujenga upya uhusiano na utangamano wa kitaifa kulingana na mwafaka wa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Kulingana na mwenyekiti mwenza wa kamati andalizi ya maombi hayo seneta wa Pokot Magharibi Samwel Poghisio hafla hii inatoa fursa kutafakari kuhusu changamoto zinazokabili taifa za ukabila na ufisadi.

Show More

Related Articles