HabariMilele FmSwahili

Serikali yapiga marufuku usafirishaji wa machine za kucheza kamare nchini

Serikali imepiga marufuku usafirishaji nchini machine za kucheza kamare. Waziri wa usalama Dr. Fred Matiangi’ amewaagiza raia wa kigeni wanaoendesha biashara hiyo nchini kuondoka mara moja. Agizo lake linajiri kufuatia msako ambao umekua ukiendelea kunasa mashine hizo ambazo nyingi zimekua zikitumika bila kusajiliwa inavyohitajika. Mapema mwaka huu,waziri aliwaagiza makamishna wa kaunti kuongoza msako huo akisema biashara hiyo imeathiri maisha ya vijana wengi baadhi wakijitoa uhai kwa kupoteza pesa zao kupitia mchezo huo.

Show More

Related Articles