HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Za Kaunti Zahimizwa Kukumbatia Mfumo Wa Kisasa Waukusanyaji Ushuru.

Ni sharti kila kaunti humu nchini kukumbatia teknologia ya kisasa ya ukusanyaji ushuru ili kuafikia azma yake ya maendeleo .

Hii ni baada ya kubainika kuwa kaunti 33 pekee ndizo zinazokusanya ushuru wake kwa njia ya kidigitali .

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ukusanyaji ushuru CRA Dr. Jane Kiringai amesema kuwa ukusanyaji ushuru katika serikali ya kitaifa na zile za kaunti bado zinakumbwa na changamoto kubwa hatua inayosambaratisha uchumi na maendeleo ya nchi .

Gavana wa Kakamega Wycliff Oparanya na gavana wa Kwale Salim Mvurya wamekiri kukumbwa na changamoto za ukusanyaji ushuru katika kipindi chao cha kwanza wakitaka kuwepo na sheria mwafaka ya ukusanyaji ushuru humu nchini .

Haya yanajiri katika kongamano la tatu la kujadili changamoto zinazokumba maswala ya ukusanyaji ushuru linaloendelea huko Diani kaunti ya Kwale .

Show More

Related Articles