People Daily

Washukiwa 30 Wa Sakata Ya NYS Wana Hadi Kesho Kujisalimisha Kwa Idara Ya Jinai.

Washukiwa 30 wanaohusishwa na sakata ya shilingi milioni 468 ya NYS wana hadi kesho saa nane mchana kujiwasilisha kwa idara ya jinai DCI licha ya washukiwa wenzao 24 kutuma maombi ya kuachiliwa kwa dhamana baada ya kufikishwa mahakamani hapo jana.

24 hao miongoni mwao katibu katika wizara ya vijana na jinsia Lillian Omollo na mkurugenzi mkuu wa NYS Richard Ndubai walikana mashtaka ya ufisadi dhidi yao walipofikishwa mbele ya hakimu Douglas Ogoti hapo jana.

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi jumanne wiki ijayo iwapo 24 hao wataachiliwa kwa dhamana au la

Show More

Related Articles