HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 33 wa sakata ya NYS kuzuiliwa rumande hadi Jumanne ijayo

Washuki 33 wa sakata ya kupotea shilingi ya shilingi bilioni 9 katika shirika la NYS wataendelea kuzuiliwa rumande hadi Jumanne ijayo. Hii ni baada ya washukiwa hao wakiwemo katibu wa masawla ya vijana Lilian Omollo na mkurugenzi mkuu wa NYS Richard Ndubai kukanusha mashitaka jana mbele ya mbele ya hakimu mkaazi Douglas Ogoti. Aidha kupitia mawakili wao washukiwa hao waliitaka mahakama kuwaachilia kwa dhamana. Upande wa mashitaka umepinga ombi hilo. Jaji Ogoti atatoa uamuzi Jumanne wiki ijayo.

Show More

Related Articles