HabariMilele FmSwahili

Raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini bila vibali wapewa hadi Julai 22 kujisajili

Raia wa kigeni wanaofanya kazi humu nchini bila vibali wamepewa hadi julai tarehe 22 kujisali lau sivyo wafurushwe. Waziri wa usalama wa taifa dkt Fred Matiangi anasema wizara yake imebaini Kenya ina zaidi ya raia wa kigeni 200,000 wanaofanya kazi nchini lakini ni 34,000 pekee waliojisajili ishara taifa linawapa makao raia wasiostahili.
Matiangi pia anataka bunge kubuni sheria itakayowalazimisha wageni wanaoingia nchini kutumia njia za mkato kutumia nauli zao kurejea nchini mwao kwani taifa linapoteza mamilioni ya pesa kuwanunulia tiketi za kuwafurusha

Show More

Related Articles