HabariPilipili FmPilipili FM News

Watoto Wa Kike Kaunti Ya Kwale Waombwa Kuzingatia Masomo Ili Kuboresha Maisha Yao

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kwale Zuleikha Hassan amewataka wanafunzi wa kike kuzingatia masomo kikamilifu badala ya kujihusisha na maswala yanayolenga kuwaharibia maisha yao ya baadae.

Zuleikha aliyekua akizungumza katika shule ya msingi ya Bang’a huko Kinango amesema elimu ndio msingi wa maisha bora itakayomaliza umaskini katika jamii za kaunti ya kwale.

Hata hivyo mwakilishi huyo ametoa  changamoto kwa  wazazi kuiga mfano wa viongozi wakike kwale walioko mamlakani  na kuhakikisha watoto wao wakike wanapata elimu bora  ili kuona kuwa  wanafaulu kimaisha badala ya kufanywa wataji katika jamii.

Show More

Related Articles