HabariMilele FmSwahili

Lilian Omolo ajisalimisha katika makao makuu ya DCI

Katibu wa masuala ya vijana aliyejiondoa afisini Lilian Omollo amejiwasilisha katika makao makuu ya DCI hapa Nairobi anakotarajiwa kuandikisha taarifa kuhusu sakata ya kupotea shilingi bilioni 9. Baada yake kudinda kufungua lango la nyumba yake eneo la Kitisuru hapa Nairobi ambapo polisi walitaka kumkamata . Omollo amejiunga na mkurugenzi wa NYS ambaye pia alijiondoa afisini na alikamatwa usiku wa kuamkia leo. Wawili hao wanajiunga na Sammy Michuki,Peter Muchui, Matano Ndoyo,James Nderitu,Yvonne Wanjiku, Sammy Mbugua, Timothy Kiplagat, Welanalo Mugubi, David Kirui, Duba Galgalo na Isaiha Dalo ambao walikamatwa usiku wa kuamkia leo wakitarajiwa kushtakiwa kuhusiana na sakata ya shilingi bilioni 9. Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji anasema wamepata ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka washukiwa hao kwa kuhusika kupora raslimali za umma.

Show More

Related Articles