HabariMilele FmSwahili

Madaktari 100 kutoka Cuba kuwasili nchini leo

Madaktari 100 kutoka nchini Cuba walioajiriwa na serikali wanatarajiwa kuwasaili nchini leo. Hii ni licha ya daktari mmoja kuwasilisha kesi mahakamani kuzuia madaktari hao kupokezwa leseni ya kuhudumu nchini. Dr Samson Robert Misango anadai kuwa hakuna ushahidi kuwa Kenya ina uhaba wa madaktari nchini. Tayari magavana wamesaini mkataba na wizara ya afya utakaowezesha madaktari kutoka Cuba kufanya kazi kaitka kaunti mbalimbali. Kila kaunti ikitarajiwa kufaidi na 2 japo watakuwa wakihamishwa kila mara kwa ufanisi bora. Kulingana na waziri wa afya Sicly Kariuki lengo sio kuwahujumu madaktari walio nchini bali kujaza uhaba uliopo hasaa mashinani.

Show More

Related Articles