HabariMilele FmSwahili

Richard Ndubai na washukiwa wengine 17 wa sakata ya NYS wakamatwa

Mkurugenzi mkuu wa shirikla la NYS aliyejiondoa Richard Ndubai kuruhusu uchunguzi wa sakata ya shilingi bilioni tisa anatarajiwa kuandikisha taarifa katika makao makuu ya DCI asubuhi hii. Ndubai pamoja na washukiwa 17 walikamatwa hapa Nairobi na mjini Naivasha usiku wa kuamkia leo. Kadhalika katibu wa maswala ya vijana lilian Omwashollo anatarajiwa kukamatwa. Haya yanajiri baada ya mkurugenzi wa mashitaka ya Noordin Hajji kuagiza washukiwa wa sakata hiyo kushitakiwa mahakamani .

Show More

Related Articles