HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wakuu Wa Sakata Ya NYS Wakamatwa.

Maafisa wanne wakuu wa shirika la NYS wamekamatwa kufuatia uchunguzi unaoendelea wa kupotea kwa shilingi bilioni 9 katika sakata ya NYS.

Wanne hao ni mkurugenzi mkuu wa NYS Richard Ndubai, msaidizi wake Sam michuki, meneja wa fedha Mbugua na afisaa mwengine wa nne ambaye jina lake halijathibitishwa.

Walikamatwa jana usiku na kufungwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Wanatarajiwa kupelekwa katika makao makuu ya DCI kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahamani ambapo watakabiliwa na mashtaka tofauti kuhusiana na sakata hiyo.

Haya yanajiri huku washukiwa wengine zaidi ya 40 wakitarajiwa kukamatwa wiki hii.

Show More

Related Articles