HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Waombwa Kuwa Imarisha Walemavu Wanao Jihusisha Na Biashara Ya Omba Omba , Mombasa

Seneta wa Kaunti ya  Mombasa Mohamed Faki amehimiza ushirikiano kati ya mashirika ya walemavu na viongozi katika  kuwa imarisha walemavu ili kukabiliana na ongezeko la walemavu wanaojihusisha na Biashara ya Omba omba.

Akizungumza na  jamii ya watu wanaoishi na ulemavu, seneta Faki amesema wapo walemavu wenye talanta na hata wasomi ambao wanafaa Kufadhiliwa ili waweze kujitegemea

Juliet Mati ambaye ni afisa Kutoka shirika la kitaifa la watu wanaoishi na ulemavu hapa mombasa, amesema wanalenga kuwatambua walemavu wote wanaojihusosha na Biashara ya Ombaomba ili kuwaanzishia miradi ya kuwakimu kimaisha.

Show More

Related Articles