HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Hoja Ya Kubadili Tarehe Ya Uchaguzi Yaibua Hisia Mseto.

Wakenya wameibua hisia mseto kuhusu pendekezo la kubadili sheria ya tarehe ya uchaguzi kutoka agosti hadi mwezi wa disemba.Baadhi wametaka tarehe ya uchaguzi isalie mwezi agosti, huku wengine wakitaka tarehe hiyo isongezwe hadi mwezi wa disemba.

Haya ni kupitia kamati ya bunge kuhusu haki na masuala ya sheria, ambayo hivi karibuni imezuru miji ya Eldoret na mombasa kukusanya maoni ya wananchi.

Katika katiba ya mwaka wa 2010 wakenya waliafikia uchaguzi uandaliwe jumanne ya pili ya mwezi agosti baada ya kila miaka mitano.Iwapo mswada uliowasilishwa na mbunge wa kiminini Chris Wamalwa utapitishwa, tarehe ya uchaguzi sasa itabadilishwa kutoka mwezi agosti, hadi jumatatu ya tatu ya mwezi wa disemba baada ya kila miaka mitano.

 

Show More

Related Articles