HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Maelfu Wajitokeza Kwa Mbio Za Mater Heart Mombasa.

Mbio za kila mwaka za Mater Heart Run zimefanyika leo katika vituo tisa humu nchini.

Katika kaunti ya mombasa Mbio hizo zimeng’oa nanga rasmi mwendo wa saa mbili kamili katika uwanja wa KPA mbaraki sports club.

Mbio hizo maalum huandaliwa kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo .

Kufikia sasa, zaidi ya watoto 3,093 wametibiwa magonjwa ya moyo, aidha kwa kufanyiwa upasuaji, pamoja na mbinu nyingine za matibabu kupitia mpango huo wa hospitali ya matter ulioanzishwa mwaka wa 1996.

Show More

Related Articles