HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wenyeji West Pokot wampa Gavana Lonyangapuo wiki 2 kumfuta naibu wake

Kutokuwepo kwa Naibu Gavana wa West Pokot Dkt. Nicholas Atudonyang kumeibua maswali mengi ikiwemo mbona gavana wa eneo hilo Prof. John Lonyangapuo hajachukua hatua yoyote.
Kwa sasa wakaazi wa kaunti hiyo wamempa Gavana Lonyangapuo wiki mbili ampige kalamu na kupata naibu mwingine atakayesaidia kuimarisha masuala ya afya katika kaunti hiyo.
Lakini kinaya ni kuwa naibu huyo anasemekana kuwa mjini Texas Marekani anapotoa huduma zake kama daktari wa upasuaji.
Aidha Gavana Lonyangapuo anadai kuwa naibu wake yuko nje ya nchi kwa shughuli rasmi zitakazo nufaisha wakaazi wake.

Show More

Related Articles