HabariMilele FmSwahili

Lilian Omollo : Hakuna fedha zilizopotea katika shirika la NYS

Katibu wa masuala ya vijana aliyejiondoa afisini Lilian Omollo sasa anasema hana ufahamu kuhusu kupotea shilingi bilioni tisa za shirika la NYS. Bi.Omollo amewaambia wabunge wa kamati ya uhasibu kwamba ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali ya mwaka 2016?/2017 iliashiria matumizi mazuri ya bajeti ya NYS na haieleweki jinsi alishindwa kutambua kupotea fedha hizo. Hata hivyo anasema anashirikiana na idara za uchunguzi kubaini iwapo kweli fedha hizo ziliporwa au la.

Bi.Omolo ambaye wakati huu anaelezea jinsi NYS ilivyobadili maisha ya vijana nchini anasema wameweka mikakati kuhakikisha matumizi mazuri ya bajeti inayotengewa shirika hilo. Aidha anasema iwapo kuna fedha zilipotea basi ni mtangulizi wake Richard Mangiti na aliyekua mkurugenzi wa NYS Nelson Githinji wanastahili kuwajibika.

Show More

Related Articles