People Daily

Shule Yafungwa Kwale Baada Ya Vyoo Kuporomoka.

Shule ya upili ya Golini  huko Matuga  kaunti ya Kwale imefungwa kwa muda  baada ya  vyoo vya shule hio kuporomoka  siku chache zilizopita kufuatia mvua inayoendelea kushuhudiwa humu nchini.

Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza tayari ametoa shilingi laki moja kwa ujenzi wa vyoo hivyo ili kuona kuwa wanafunzi hawasalii nyumbani.

Akizungumza  wakati wa kupeana fedha hizo Tandaza amewataka  wanafunzi  haswa wale wakidato cha nne kurudi  shuleni  mara moja na kuendelea na masomo ikizingatiwa kuwa kukaa kwao kwa nyumbani huenda kukazorotesha viwango vyao  vya elimu.

Show More

Related Articles