HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika: Tunamtambua mwalimu mstaafu anayeshauri kuhusu malezi ya vijana

Wataalamu wa malezi ya watoto wachanga husema, kutumia muda wako kama mzazi na mwanao, huchangia pakubwa kwenye tabia njema na ufanisi wa mtoto.

Hata hivyo, majukumu ya uzazi yameachiwa walimu shuleni na marafiki ambao watoto hutangamana nao maishani hali ambayo Bi Lizzie Wanyoike, mshauri wa masuala ya uzazi na malezi anawakanya wazazi wa sasa.

Kwenye makala ya Wasiotambulika wiki hii, tunaitambua bidii ya Bi Lizzie Wanyoike aliyejitolea kuwashauri vijana na wazazi kila mara anapokutana nao huku akilenga kuona kwamba kizazi kijacho hakiambulii gizani.

Show More

Related Articles